Gladbach yachelewesha karamu ya Bayern
Bayern Munich inasubiri hadi wikendi ijayo. Bayern ilitoka sare ya bao moja kwa moja na Borussia Moenchengladbach, wakati Borussia Dortmun...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/gladbach-yachelewesha-karamu-ya-bayern.html
Bayern Munich inasubiri hadi wikendi ijayo. Bayern ilitoka sare ya bao
moja kwa moja na Borussia Moenchengladbach, wakati Borussia Dortmund
ikiendeleza shinikizo kwa kuibambua Wolfsburg 5-1
Hata hivyo, beki wa Dortmund Mats Hummels alikuwa na wakati mgumu
uwanjani baada ya baadhi ya mashabiki kumpigia kelele tangu alipotangaza
kuwa angetaka kujiunga na Bayern Munich. Na baada ya mechi, Hummels
alisema "Hiyo yote ni jazba, nandivyo ilivyo kwangu pia. Lakini uwanjani
lazima uyaweke hayo yote kando na ndivyo nilivyofanya. Nadhani leo
nimesaidia katika ushindi wetu pia tumekuwa na msimu mzuri. Hivyo, kwa
jumla yote yamekwenda sawa".Matokeo hayo yalilipunguza pengo kati yao na Bayern kuwa pointi tano huku kukiwa na mechi mbili msimu kukamilika maana kuwa vijana hao wa Pep Guardiola hawangetawazwa mwishoni mwa wiki kuwa washindi wa taji lao la nne mfululizo la Bundesliga na lao la 26 kwa ujumla.
Bayer Leverkusen ilijihakikishia nafasi ya tatu na hivyo tikiti ya moja kwa moja ya Champions League kwa kuipiku Hertha Berlin 2-1 ambao wamedondoka kutoka nafasi za Champions League. Julian Brandt aliifungia Leverkusen bao katika mchuano wake wa sita mfululizo. "Nadhani kama mtu angetuambia miezi minne kabla kuwa mwishoni mwa msimu tungemaliza nafasi ya tatu ikiwa imesalia wiki mbili, kila mmoja angeweza kusaini tukiwa tumefunga macho. Ndio maana sote tuna furaha kubwa. Tumeshusha pumzi na unaweza kuona hilo kwenye nyuso zetu".
Kwingineko, Eintracht Frankfurt walijipa matumaini ya kuepuka kushushwa daraja kwa kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Darmstadt ambao wamo hatarini. Hoffenheim waliimarisha matumaini ya kusalia katika Bundesliga baada ya kutoka nyuma na kuibwaga Ingolstadt 2-1.
Schalke ilisonga hadi nafasi ya sita ikiwa ni fursa ya kucheza kandanda la Europa Legaue, kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Hanover ambao tayari walishushwa daraja. Mainz walisonga hadi nafasi ya saba kwa kutoka sare tasa na Hamburg
Leo usiku, Werder Bremen watashuka dimbani na Stuttgart katika mchuano mgumu wa vita vya kuepuka kushuka daraja. Ni mara ya kwanza ambapo Bundesliga imeandaa mchuano siku ya Jumatatu usiku, utaratibu ambao unatarajiwa kuanza kutekelezwa msimu ujao. Mashabiki wa Bremen wanapanga kususia mchuano huo