Jamie Vardy ndiye mwanasoka bora wa mwaka
Mshambuliaji wa klabu ya Leicester City Jamie Vardy ametangazwa mshindi wa tuzo ya mwana soka bora wa mwaka na chama cha waandishi wa kand...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/jamie-vardy-ndiye-mwanasoka-bora-wa.html
Mshambuliaji wa klabu ya Leicester City Jamie Vardy ametangazwa mshindi
wa tuzo ya mwana soka bora wa mwaka na chama cha waandishi wa kandanda
Uingereza
Mshambuliaji huyo wa Uingereza alipata asilimia 36 ya kura zilizopigwa
na wanahabari 290 na kuwapiku wenzake Riyad Mahrez na N'Golo Kante.
Vardy mwenye umri wa miaka 29, amefunga mabao 22 ya ligi kuu ya kandanda
England.Pia alivunja rekodi ya kufunga mabao kila mechi katika mechi 11 mfululizo. Leicester City inahitaji pointi mbili pekee ili kushinda Ligi Kuu ya England lakini inaweza pia kutawazwa mabingwa iwapo Tottenham Hotspurs watashindwa kuwalaza Chelsea leo usiku.
Riyad Mahrez raia wa Morocco alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya PFA, ambayo mshindi hupigiwa kura na wachezaji soka ya kulipwa