Iran yaitaka Marekani kufidia uhalifu
Bunge nchini Iran Bunge la Iran limepitisha sheria inayoitaka serikali kuitisha fidia kutoka Marekani kwa uhalifu ul...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/iran-yaitaka-marekani-kufidia-uhalifu.html
![]() |
Bunge nchini Iran |
Bunge la Iran limepitisha sheria
inayoitaka serikali kuitisha fidia kutoka Marekani kwa uhalifu
uliotendwa kwa zaidi ya miaka 60.
Kati ya vitendo vilivyotajwa kwenye sheria hiyo ni mapinduzi ya mwaka 1953 ambayo yaliiangusha serikali ya Mohammad Mossadegh.Mahakama ya juu zaidi nchini Marekani hivi majuzi iliamua kuwa Iran ni lazima iwalipe fidia ya karibu dola bilioni mbili waathiriwa wa mashambulizi ambayo Marekani inadai yalisababishwa na Iran.
Hii inajumuisha mashambulizi ya kambi ya jeshi la Marekani mjini Beirut mwaka 1983.