Leicester City kunyemelea ushindi Epl?
Leicester City imetoka sare ya 1-1 ilipokutana na Manchester United Leicester City wamebakiwa na alama mbili pekee kuu...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/leicester-city-kunyemelea-ushindi-epl.html
![]() |
Leicester City imetoka sare ya 1-1 ilipokutana na Manchester United |
Leicester City wamebakiwa na alama
mbili pekee kuupata ushindi wa ligi kuu ya England baada ya kupata sare
ya 1-1 dhidi ya klabu ya Manchester United katika dimba la Old Trafford
huku wakitegemea matokeo ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Tottenham
utakaopigwa leo hii majira ya saa nne usiku kwa saa za afrika mashariki
katika dimba la Stamford Bridge.
kwa matokeo hayo Leicester wanaendelea kubaki kileleni mwa ligi ya England wakiwa na alama 77.
Claudio Ranieri huyo akisisitiza kuwa hawakufuata kikombe OT bali kucheza mchezo safi lakini Man U walikua wazuri zaidi yao. Matokeo mengine Liverpool walikiona cha mtema kuni baada ya kuchapwa 3-1 walipokuwa wageni wa Swansea huku Man city wakiambulia kichapo cha mbwa mwizi 4-2 walipowatembelea Sauthampton.