Mcheza Tenisi Grigor Dimitrov aomba radhi

Grigor amepoteza mchezo alipokua akisaka taji lake la kwanza Mcheza tenisi wa Bulgaria Grigor Dimitrov ameomba radhi baada ya kuonyes...

Grigor amepoteza mchezo alipokua akisaka taji lake la kwanza
Mcheza tenisi wa Bulgaria Grigor Dimitrov ameomba radhi baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu pale alipoibamiza chini mara tatu fimbo yake ya kuchezea baada ya kukubali kichapo dhidi ya Diego Schwartzman katika michuano ya wazi ya Istanbul.
Mbulgaria huyo aliyekuwa akilisaka taji lake la kwanza katika kipindi cha miaka miwili alipoteza kwa seti 6-7,5-7,7-6, 7-4,na 6-0.
Dimitrov alipewa onyo kali aliporusha kwa mara ya kwanza na kwa hasira fimbo yake ya kuchezea mapema mnamo seti ya tatu na kisha akapewa adhabu kwa kurudia tukio hilo. Huku akiwa nyuma kwa seti 5-0,alifanya tena kosa kama hilo na kumpa mpinzani wake ushindi wa wazi.
''Nimeiangusha familia yangu,Timu yangu,mashabiki wangu kwa tabia mbaya ambayo kwa kweli ninaomba radhi''alisema mchezaji huyo nambari 29 duniani katika mchezo wa tenisi.
Nidhamu ya mchezaji huyo mwenye miaka 24 ilimpatia ushindi na kikombe Schwartzman mwenye miaka 23 katika michuano hiyo aliyoshiriki kwa mara ya kwanza.

Related

MICHEZO 1570715547137841559

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item