Maandamano ya kumpinga Kabila yafanyika DRC
Maandamano ya upinzani yanafanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupinga uamuzi wa mahakama ya kikatiba mapema mwezi huu k...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/maandamano-ya-kumpinga-kabila-yafanyika.html
Maandamano ya upinzani yanafanyika
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupinga uamuzi wa mahakama ya
kikatiba mapema mwezi huu kwamba rais Joseph kabila atasalia madarakani
baada ya mda wake kukamilika iwapo uchaguzi hautafanyika mwishoni mwa
mwaka huu.
Maandamano hayo yamepigwa marufuku katika maeneo
mengine ikiwemo mji wa Lubumbashi nyumbani kwa mgombea wa urais wa
Upinzani Moise Katumbi.Mashariki mwa mji wa Goma hali inazidi kuwa mbaya ,huku waandishi wa habari wakituma ujumbe wa Twitter kwamba jeshi limekuwa likifyatua risasi na kuwazuia raia kukongamana.
Mwandishi huru wa habari Ley Uwara alituma ujumbe wa Twitter kwa lugha ya Ufaransa kwamba hakuna uchukuzi wa umma hivyobasi watu wameshindwa kwenda kazini.

Anasema kuwa baadhi ya vijana wamekamatwa na jeshi kutumwa ili kuwasaidia maafisa wa polisi