Manchester City wachapwa na Real Madrid
Gareth Bale alifungia Real bao la pekee mechi hiyo Manchester City wameshindwa kufika katika fainali za kwanza za klabu bingwa bara...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/manchester-city-wachapwa-na-real-madrid.html
![]() |
Gareth Bale alifungia Real bao la pekee mechi hiyo |
Manchester City wameshindwa kufika
katika fainali za kwanza za klabu bingwa barani Ulaya (UEFA) baada ya
kutolewa na mabingwa mara 10 wa michuano hiyo Real Madrid katika mchezo
uliokua wa kuvutia tena wa aina yake. Walichapwa 1-0.
Baada ya
kutokuwa na ushindi wowote katika mzunguko wa kwanza, Real Madrid
walianza kuongoza kipindi cha kwanza kufuatia mpira wa krosi uliopigwa
na Gareth Bale kumbabatiza kiungo wa City Fernando na kuingia nyavuni.Real waliutawala mchezo huku mpira wa kichwa uliopigwa na Bale ukigonga mwamba na baadaye mlinda mlango wa City Joe Hart akiondoa mikwaju ya Luka Modric na Cristiano Ronaldo.

Madrid walipata wakati mgumu kidogo pale mkwaju mkali wa Sergio Aguero ulipogonga nyavu za juu za lango la Madrid. Real sasa watakutana na Atletico katika uwanja wa San Siro tar 28 Mei, hii ikiwa ni kama marudio ya fainali za mwaka 2014 ambapo Real walishinda kwa mabao 4-1 baada ya muda wa nyongeza.