Ranieri awataka nyota wake kusalia
Ranieri Meneja wa kilabu ya leicester Claudio Ranieri amewataka nyota wake kati...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/ranieri-awataka-nyota-wake-kusalia.html
![]() |
Ranieri |
Meneja wa kilabu ya
leicester Claudio Ranieri amewataka nyota wake katika kikosi chake
kusalia katika timu hiyo kwa mwaka mmoja zaidi.
Mbweha hao waliwashangaza wengi kwa kushinda ligi hiyo baada ya kutumia pauni milioni 57 pekee msimu huu.Winga Riyad Mahrez ,mshambuliaji Jamie Vardy na kiungo wa kati N'golo Kante ni miongoni mwa wachezaji wa klabu hiyo wanaotarajiwa kuondoka na kujiunga na timu nyengine msimu ujao.
''Nina matumaini tele'',alisema Ranieri.''Musiende''.

Wahandishi wa habari walimpatia heshima kwa kusimama kocha huyo wa Itali aliyechukua mahala pake Nigel Pearson msimu uliopita wakati alipowasili kwa mkutano na vyombo vya habari.