'Maria Sharapova huenda asicheze tena'

Maria sharapovu Aliyekuwa mchezaji nambari moja wa tenisi kwa upande wa wanawake Maria Sharapova huenda asicheze tena baada ya kubain...

Maria sharapovu

Aliyekuwa mchezaji nambari moja wa tenisi kwa upande wa wanawake Maria Sharapova huenda asicheze tena baada ya kubainika kwamba amekuwa akitumia dawa za kusisimua misuli, rais wa shirikisho la mchezo wa tenisi nchini Urusi amesema.
Raia huyo wa Urusi mwenye umri wa miaka 29 alipatikana na dawa ya Meldonium katika michano ya Australia Open mnamo mwezi Januari.
Alipoulizwa iwapo Sharapova atashiriki katika michuano mengine,Shamil Tarpishchev aliambia kitengo cha habari cha R-Sport kwamba hadhani, akiongezea kwamba mshindi huyo mara tano wa Grand Slam alikuwa katika hali mbaya.
Mnamo mwezi Machi,Sharapova alisema kuwa alikuwa tayari kuendelea na tenisi.
Shirikisho la kimataifa la mchezo wa tenisi ITF lilimpiga marufuku kwa mda Sharapova mnamo tarehe 12 mwezi Machi.
Anasubiri kusikia adhabu yake kamili ,ambayo huenda ikawa marufuku ya miaka minne,ijapokuwa wataalam wanasema huenda akapewa marufuku ya miezi sita au 12.

Related

MICHEZO 6916274431417372306

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item