Rio :IOC kuwapiga marufuku wanariadha 31
Rio Olimpiki Hadi wanariadha 31 kutoka michezo sita tofauti huenda wakapigwa marufuku kutoshiriki katika michezo ya Olimpiki, kul...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/rio-ioc-kuwapiga-marufuku-wanariadha-31.html
![]() |
Rio Olimpiki |
Hadi wanariadha 31 kutoka michezo
sita tofauti huenda wakapigwa marufuku kutoshiriki katika michezo ya
Olimpiki, kulingana na maafisa wa mashindano hayo.
Tangazo hilo linajiri baada ya kamati ya kimataifa ya Olimpiki kukagua violezi kutoka kwa michezo ya Olympiki ya Beijing 2008.Kamati hiyo ya IOC imesema kuwa vipimo hivyo vilikaguliwa kwa kutumia teknolojia mpya ya kisayansi .
Pia imebaini kwamba inangojea matokeo vipimo vyengine 250 kutoka kwa michezo ya Olympiki ya mwaka 2012 mjini London.
''Mikakati yote hii inalenga kuwazuia wanaodanganya kutoshinda'',rais wa wa IOC Thomas Bach alisema.

''Tunaweka violezo kwa miaka 10 ili wadanganyifu wajue kwamba hatutachoka''.
''Kwa kuwazuia wale waliodanganya kushiriki mjini Rio,tunaonyesha kwa mara nyengine kwamba tunaweka juhudi za kulinda maadili ya mashindano haya ya Olympiki''.