Serengeti boys kushuka dimbani leo
Timu ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’inashuka dimbani leo kuchuana na Malaysia.Mchezo huu utap...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/serengeti-boys-kushuka-dimbani-leo.html
Timu ya Tanzania ya vijana chini ya
umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’inashuka dimbani leo kuchuana
na Malaysia.Mchezo huu utapigwa katika uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa
India ikiwa ni mchezo wa kuwania nafasi ya tatu kwenye michuano maalumu
ya kimataifa yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF
Youth Cup 2016 U-16).
Katika mchezo wa kuwania kucheza fainali,
Serengeti Boys iliruhusu sare ya mabao 2-2 Malaysia hivyo kufikisha sare
ya tatu baada ya kushinda mechi moja.Serengeti Boys imemaliza hatua ya
awali ikiwa na pointi sita sawa na Korea Kusini, lakini ikazidiwa bao
moja hivyo kushika nafasi ya tatu katika michuano ambayo Marekani
iliongoza kwa kufikisha alama nane.India kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.