Vijana wa Serengeti boys Timu ya soka ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' leo Mei 19, 2016 ime...
http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/tanzania-yatoka-sare-na-korea-kusini.html
 |
Vijana wa Serengeti boys |
Timu ya soka ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
'Serengeti Boys' leo Mei 19, 2016 imetinga hatua ya nusu fainali baada
ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea Kusini katika mfululizo wa michuano
maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo
(AIF Youth Cup 2016 U-16). Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa
Tilak, Maidan mjini Goa, India, mabao ya Serengeti yalifungwa na Assad
Juma katika dakika ya 12 na Maulid Lembe katika dakika ya 87 ambaye
alisawazisha baada ya Korea kutangulia kwa mabao 2-1. Matokeo hayo
yanaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi tano na kwamba inasubiri
matokeo ya mwisho kati ya Korea Kusini na Marekani yatakayotoa mwanga wa
timu itakayocheza fainali. Serengeti Boys watashuka dimbani tena dhidi
ya Malaysia Mei 21, 2016,Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25, 2016
na kabla ya mchezo wa fainali, utachezwa mchezo wa mshindi wa tatu
katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa nchini India. India
imeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya fainali za kombe la
dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017