'Mvulana wa Messi'' atorokea Pakista
messi Mvulana mwenye umri wa miaka 5 ambaye picha yake ilisambaa katika mitandao ya kijamii akiwa amevalia shati ya Lionel Messi a...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/mvulana-wa-messi-atorokea-pakista.html
![]() |
| messi |
Mvulana mwenye umri wa miaka 5
ambaye picha yake ilisambaa katika mitandao ya kijamii akiwa amevalia
shati ya Lionel Messi ametorokea nchini Pakistan.
Babaake Murtza Ahmadi amesema kuwa alipata vitisho vya kutekwa nyara ikiwemo kutoka kwa wahuni waliokuwa wakitaka pesa.Baada ya mvulana huyo kuwa maarufu kutokana na shati yake yenye mistari ya bluu,nyota huyo wa Argentina alimpatia jezi mbili alizozitia saini pamoja na mpira.''Nampenda Messi''.
''Ni mfalme'',Murtaza ambaya ana matumaini ya kuonana naye aliiambia BBC.Babaake Murtaza anasema kuwa waliondoka nyumbani kwao huko Ghazni kwa sababu hali ilikuwa hatari kwake.
Sasa familia inahisi kwamba Quetta itatoa makaazi mazuri kwa maisha ya Murtaza na ndugu zake saba ambao wote wanalala chumba kimoja.



