Whatsapp yafungwa kwa saa 72 Brazil
Hakimu mmoja nchini Brazili amefunga mawasiliano ya mtandano wa simu kwa njia ya whatsapp kwa saa 72.Hakimu huyo Marcel Montalvao amese...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/whatsapp-yafungwa-kwa-saa-72-brazil.html
Hakimu mmoja nchini
Brazili amefunga mawasiliano ya mtandano wa simu kwa njia ya whatsapp
kwa saa 72.Hakimu huyo Marcel Montalvao amesema kampuni inayomiliki
mtandao huo imeshindwa kusaidia kutoa taarifa katika kesi ya uhalifu.
Mwezi
Machi,Montalvao aliamuru kukamatwa kwa afisa mwandamizi wa Facebook
katika nchi za Kilatini bwana Diego Dzoran baada ya kukataa kutoa
ushirikiano katika uchunguzi dhidi ya dawa za kulevya.Whatsapp mtandao unaomilikiwa na Facebook umesema umekatishwa tamaa na kitendo hicho kwa kuwa wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha mahakamani.
Mtandao huo umekuwa ukifungiwa mara kadhaa nchini Brazil kwa miezi michache ya karibuni kwa sababu zinazofanana na hizo.



