Ndege zashambulia barabara karibu na Allepo, Syria
Ndege zilifanya mashambulizi kwenye barabara inayoelekea maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mji wa Allepo. Wanahara...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/ndege-zashambulia-barabara-karibu-na.html
![]() |
| Ndege zilifanya mashambulizi kwenye barabara inayoelekea maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mji wa Allepo. |
Wanaharakati nchini Syria wanasema
kuwa ndege za kivita zimefanya mashambulizi makubwa zaidi kwenye
barabara inayoelekea maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mji wa
Allepo.
Wanaharakati wanasema kuwa ndege za Urusi na za serikaliya
Syria, zimeshirika kwenye mashambulizi hayo licha ya hilo
kutothibitishwa rasmi.Serikali ya Syria imekuwa ikishambulia maeneo yanayodhibitiwa na waasi mjini Allepo siku za hivi karibuni na kuvunja makubaliano yaliyoafikiwa mwishoni mwa mwezi Februari.



