Barcelona: Tunakabiliwa na upinzani mkali
Klabu ya Barcelona italazimika kushinda mechi zake zote za mwisho ili kushinda taji la ligi ya La Liga kwa kuwa huenda wapinzani ...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/barcelona-tunakabiliwa-na-upinzani-mkali.html
Klabu ya Barcelona italazimika
kushinda mechi zake zote za mwisho ili kushinda taji la ligi ya La Liga
kwa kuwa huenda wapinzani wao wasipoteze hata pointi moja kulingana na
kocha Kuis Enrique.
Viongozi Barcelona walioanza mwezi wa April
wakiwa na pointi nane kileleni mwa ligi hiyo,wako sawa kwa pointi na
Atletico Madrid huku Real Madrid ilio nafasi ya tatu wakiwa nyuma kwa
pointi moja.''Haiwezekani kwamba timu zilizo nyuma yetu zitapoteza pointi'',alisema Enrique siku ya Ijumaa.

Barcelona iko mbele ya Atletico kutokana na tofauti ya mabao.
Barca,Atletico na Real Madrid zote zinacheza Jumamosi katika muda tofauti.
