Mwanamke mtumwa kuwekwa kwenye dola Marekani

Tubman alizaliwa utumwani jimbo la Maryland. Picha ya mtumwa mmoja aliyekata nyororo na kisha kusaidia mamia ya wenzak...

Tubman alizaliwa utumwani jimbo la Maryland.
Picha ya mtumwa mmoja aliyekata nyororo na kisha kusaidia mamia ya wenzake kutoroka utumwa sasa itatumika katika noti mpya ya dola 20 nchini Marekani.
Bi Harriet Tubman atakuwa Mwafrika Mmarekani wa kwanza kuangaziwa kwenye sarafu ya Marekani.
Vilevile ndiye mwanamke wa kwanza katika kipindi cha karne moja katika historia ya Marekani picha yakwe kuwekwa kwenye dola.
Picha hiyo itabadilishwa na ile ya awali ya rais wa saba wa Marekani Andrew Jackson ambaye alikuwa akimiliki watumwa enzi hizo.
Sasa picha ya Andrew Jackson itakuwa nyuma ya noti hiyo.
Noti hiyo itaanza kutumika mwaka 2020 lakini idara ya fedha nchini Marekani imesema ni mwanzo wa kuwakumbuka na kuwaenzi waliopigania haki za kibinadamu nchini humo.
Bi Tubman alizaliwa miaka ya 1800 utumwani jimbo la Maryland. Alifariki 10 Machi, 1913 akiwa eneo la Auburn, jimbo la New York.

Related

MATUKIO 7084028030458513271

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item